Majukumu Ya Bodi Ya Pamba Tanzania Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Pamba Na. 2 Ya Mwaka 2001
2. Kuongeza uzalishaji na uchambuaji wa pamba pamoja na kuboresha masoko ya pamba
3. Kusimamia na kudhibiti ununuzi wa pamba mbegu na nyuzi kuanzia ngazi ya gulio, kiwandani na masoko
4. Kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu uzalishaji wa pamba, uchambuaji na masoko
5. Kukusanya, kuainisha na kueneza taarifa zinazohusu pamba na kuimarisha matumizi ya taarifa hizo na kuziendeleza kwa ajili ya kuimarisha zao la pamba
6. Kuwaruhusu wanunuzi na wauzaji wa pamba wenye viwanda vya kuchambua pamba na kupanga sifa na masharti ya leseni
7. Kutoa vibali vya kuuza pamba nyuzi nje na kupanga masharti ya kutoa vibali hivyo
8. Kupanga viwango vya madaraja ya pamba mbegu na pamba nyuzi na kuhakikisha kuwa viwango hivyo vinafuatwa
9. Kupanga utaratibu wa kiasi cha mbegu za kupanda ambacho kila mnunuzi wa pamba mbegu atatenga kwa ajili ya kupanda.
10. Kuiwakilisha serikali na wakulima katika mikutano yote ya kimataifa inayoihusu pamba
Bodi ya pamba kama chombo cha usimamizi hairuhusiwi kufanya shughuli yoyote ya kibiashara isipokuwa tu pale inapopewa kibali na waziri kwa muda maalum.





